Kupro
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kupro (pia: Kipro, Kuprosi, na hata Saiprasi kutoka Kiingereza Cyprus) ni nchi ya kisiwani upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: none | |||||
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν imnos is tin eleftherian Utenzi wa uhuru1 | |||||
Mji mkuu | Nikosia | ||||
Mji mkubwa nchini | Nikosia | ||||
Lugha rasmi | Kigiriki, Kituruki | ||||
Serikali | Jamhuri Nicos Christodoulides | ||||
Uhuru Tarehe |
16 Agosti 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
9,251 km² (ya 162) 9 | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
1,244,188 (ya 158) 838,897 123.4/km² (ya 82) | ||||
Fedha | Cyprus Pound (CYP ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .cy3 | ||||
Kodi ya simu | +357
- | ||||
1 Sawa na wimbo la taifa la Ugiriki |
Kijiografia ni sehemu ya Asia, lakini kiutamaduni na kisiasa ni sehemu ya Ulaya.
Watu waliishi huko walau kuanzia milenia ya 10 KK.
Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa hicho.
Kisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko.
Kuanzia mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji mizima.
Baada ya Wakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu, Waturuki Waosmani walikiteka mwaka 1570 na kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya awali.
Mwaka 1878 Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914.
Tarehe 16 Agosti 1960 Kupro ilijipatia uhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana na Ugiriki au kugawiwa kati ya kaskazini (Waturuki) na kusini (Wagiriki).
Tangu vita vya Kupro, 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa yanatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.
Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004.
Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kigiriki, wengine Kituruki, ambazo zote mbili ni lugha rasmi.
Kwa jumla hao wa kwanza ni Wakristo (72.3% za wakazi wote), wa pili ni Waislamu (25%).
Wakristo karibu wote ni Waorthodoksi; wengine ni Wakatoliki (2.9%, hasa Wamaroni), Waprotestanti (2%) na Waarmenia.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.