Iota (pia: yodi) ni herufi ya tisa katika Alfabeti ya Kigiriki. Umbo la iota kubwa na ndogo limeendelea vilevile katika alfabeti ya Kilatini na hivyo hutumiwa vile hadi leo katika lugha zote zinazotumia mwandiko huo kama vile Kiswahili, Kiingereza na kadhalika.

Ukweli wa haraka Alfabeti ya Kigiriki, Herufi za kawaida ...
Funga

Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 10.[1]

Matamshi yake ni sawa na "i" kwa Kiswahili.

Neno iota = yodi katika tafsiri ya Biblia

Katika tafsiri ya Biblia ya "Union Bible" neno "yodi" hutumiwa pale ambako lugha asilia ya Kigiriki inatumia "iota" .

Math 5:18: Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie. [2]

Hapa neno iota/yodi hutumiwa kumaanisha "herufi ndogo kabisa" yaani sehemu ndogo yoyote ya Maandiko matakatifu.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.