Sigma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sigma (Σ σ ς) ni herufi ya 18 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama σ (alama ya kawaida) au Σ (alama kubwa mwanzoni mwa majina). Kama iko mwishoni mwa neno huandikwa ς. Mfano jina Ὀδυσσεύς (Odysseus) ambamo kuna σ mbili katikati na ς mwishoni.
Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu, ikiwa alama ya namba 200.
Asili ya sigma ni herufi ya Kifinisia ya shin 𐤔 .
Matamshi yake ilikuwa "s".
Katika alfabeti zinazofuata mfano wa Kigiriki ilipokelewa katika alfabeti ya Kilatini kama "S" na katika alfabeti ya Kisirili kama "С".
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads