Omega
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Omega, yaani "o kubwa" (Ω ω) ni herufi ya ishirini na nne pia ya mwisho katika alfabeti ya Kigiriki.
Jina la Kigiriki lamaanisha "O kubwa" kwa kuitofautisha na Omikron au "O ndogo". Maana matamshi ya omega ilikuwa "oo" (o ndefu).
Alama yake ilikuwa pia na maana ya namba 800.
Katika sayansi omega hutumiwa hasa kama alama ya omu (Ohm) yaani kipimo cha ukinzani wa umeme.
Omega ikiwa herufi ya mwisho ya alfabeti ya Kigiriki, hutumiwa mara nyingi kwa kutaja mwisho. Hivyo ni kinyume cha mwanzo au alfa.
Usemi wa Biblia hujulikana kuhusu Mungu kuwa "Alfa na Omega, mwanzo na mwisho" (Ufunuo wa Yohane 21:6).
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads