Ksi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ksi (Ξ ξ) ni herufi ya 14 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama ξ (alama ya kawaida) au Ξ (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu ikiwa alama ya namba 60.
Asili ya ksi ni herufi ya Kifinisia "samekh" . Herufi zilizotokana nayo katika alfabeti zilizofuata Kigiriki ni X katika alfabeti ya baadhi ya lugha za Kirumi na Ksi (Ѯ, ѯ) katika alfabeti ya Kisirili.
Matamshi yake ilikuwa "ks".
Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, ξ inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads